Zaburi 150

Neno: Kiswahili Contemporary Version

Msifuni Bwana. Msifuni Mungu katika patakatifu pake, msifuni katika mbingu zake kuu.

Msifuni kwa matendo yake makuu, msifuni kwa kadiri ya wingi wa ukuu wake.

Msifuni kwa mvumo wa tarumbeta, msifuni kwa kinubi na zeze,

msifuni kwa matari na kucheza, msifuni kwa kinanda cha nyuzi na filimbi,

msifuni kwa matoazi yaliayo, msifuni kwa matoazi yavumayo sana.

Kila chenye pumzi na kimsifu Bwana. Msifuni Bwana!

Zaburi

Fungua msomaji shirikishi ili kubadilisha tafsiri, kurekebisha herufi, na kutia alama mistari — au vinjari mistari kwa mada.

Neno: Bibilia Takatifu — Kiswahili Contemporary Version. Copyright © 1984, 1989, 2009, 2015 Biblica, Inc. Used under the Biblica Open (Toleo Wazi) License. · Biblica Open License