Zaburi 120

Open Word Bible

Wimbo wa kupanda. Nilipokuwa katika taabu nilimlilia BWANA, naye akanijibu. Ee BWANA, uniokoe na watu ambao midomo yao husema uongo, ambao ndimi zao hudanganya. Ewe ulimi wa udanganyifu, atakupa nini, na atakuzidishia nini zaidi? Mishale mikali ya mpiganaji hodari, na makaa ya moto ya mti wa mretemu! Ni taabu kwangu, kuishi kama mgeni huko Mesheki, kufanya makao yangu kati ya mahema ya Kedari! Kwa muda mrefu mno nimelazimika kuishi karibu na watu wanaochukia amani. Mimi ninasimama upande wa amani, lakini ninapofungua kinywa changu, wao wanachagua vita.

Zaburi

Fungua msomaji shirikishi ili kubadilisha tafsiri, kurekebisha herufi, na kutia alama mistari — au vinjari mistari kwa mada.

Manukuu ya Maandiko yametoka katika Open Word Bible, ambayo iko katika uwanja wa umma.