Zaburi 128

Neno: Kiswahili Contemporary Version

Heri ni wale wote wamchao Bwana, waendao katika njia zake.

Utakula matunda ya kazi yako; baraka na mafanikio vitakuwa vyako.

Mke wako atakuwa kama mzabibu uzaao ndani ya nyumba yako; wana wako watakuwa kama machipukizi ya mizeituni kuizunguka meza yako.

Hivyo ndivyo atakavyobarikiwa mtu amchaye Bwana.

Bwana na akubariki kutoka Sayuni siku zote za maisha yako, na uone mafanikio ya Yerusalemu,

nawe ujaliwe kuishi uone watoto wa watoto wako. Amani iwe juu ya Israeli.

Zaburi

Fungua msomaji shirikishi ili kubadilisha tafsiri, kurekebisha herufi, na kutia alama mistari — au vinjari mistari kwa mada.

Neno: Bibilia Takatifu — Kiswahili Contemporary Version. Copyright © 1984, 1989, 2009, 2015 Biblica, Inc. Used under the Biblica Open (Toleo Wazi) License. · Biblica Open License