Zaburi 124

Neno: Kiswahili Contemporary Version

Kama Bwana asingalikuwa upande wetu; Israeli na aseme sasa:

kama Bwana asingalikuwa upande wetu, wakati watu walipotushambulia,

wakati hasira yao ilipowaka dhidi yetu, wangalitumeza tungali hai,

mafuriko yangalitugharikisha, maji mengi yangalitufunika,

maji yaendayo kasi yangalituchukua.

Bwana asifiwe, yeye ambaye hakuruhusu turaruliwe kwa meno yao.

Tumeponyoka kama ndege kutoka mtego wa mwindaji; mtego umevunjika, nasi tukaokoka.

Msaada wetu ni katika jina la Bwana, Muumba wa mbingu na dunia.

Zaburi

Fungua msomaji shirikishi ili kubadilisha tafsiri, kurekebisha herufi, na kutia alama mistari — au vinjari mistari kwa mada.

Neno: Bibilia Takatifu — Kiswahili Contemporary Version. Copyright © 1984, 1989, 2009, 2015 Biblica, Inc. Used under the Biblica Open (Toleo Wazi) License. · Biblica Open License