Zaburi 61

Neno: Kiswahili Contemporary Version

1Ee Mungu, sikia kilio changu, usikilize maombi yangu.

2Kutoka miisho ya dunia ninakuita, ninaita huku moyo wangu unadhoofika; uniongoze kwenye mwamba ule ulio juu kuliko mimi.

3Kwa kuwa umekuwa kimbilio langu, ngome imara dhidi ya adui.

4Natamani kukaa hemani mwako milele, na kukimbilia chini ya uvuli wa mbawa zako.

5Ee Mungu, kwa kuwa umesikia nadhiri zangu, umenipa urithi wa wale wanaoliogopa jina lako.

6Mwongezee mfalme siku za maisha yake, miaka yake kwa vizazi vingi.

7Yeye na atawazwe kwenye kiti cha enzi mbele za Mungu milele; amuru upendo wako na uaminifu wako vimlinde.

8Ndipo daima nitaliimbia sifa jina lako na kuzitimiza nadhiri zangu siku baada ya siku.

Zaburi

Open the interactive reader to switch translations, adjust type, and mark verses — or browse verses by topic.

Neno: Bibilia Takatifu — Kiswahili Contemporary Version. Copyright © 1984, 1989, 2009, 2015 Biblica, Inc. Used under the Biblica Open (Toleo Wazi) License. · Biblica Open License