Zaburi 126

Neno: Kiswahili Contemporary Version

Bwana alipowarejeza mateka Sayuni, tulikuwa kama watu walioota ndoto.

Vinywa vyetu vilijaa kicheko, ndimi zetu zilijaa nyimbo za shangwe. Ndipo iliposemwa miongoni mwa mataifa, “ Bwana amewatendea mambo makuu.”

Bwana ametutendea mambo makuu, nasi tumejaa furaha.

Ee Bwana, turejeshee watu wetu waliotekwa, kama vijito katika Negebu.

Wapandao kwa machozi watavuna kwa nyimbo za shangwe.

Yeye azichukuaye mbegu zake kwenda kupanda, huku akilia, atarudi kwa nyimbo za shangwe, akichukua miganda ya mavuno yake.

Zaburi

Fungua msomaji shirikishi ili kubadilisha tafsiri, kurekebisha herufi, na kutia alama mistari — au vinjari mistari kwa mada.

Neno: Bibilia Takatifu — Kiswahili Contemporary Version. Copyright © 1984, 1989, 2009, 2015 Biblica, Inc. Used under the Biblica Open (Toleo Wazi) License. · Biblica Open License