Zaburi 11

Neno: Kiswahili Contemporary Version

1Kwa Bwana ninakimbilia, unawezaje basi kuniambia: “Ruka kama ndege kwenye mlima wako.

2Hebu tazama, waovu wanapinda pinde zao, huweka mishale kwenye uzi wake, wakiwa gizani ili kuwapiga wale wanyofu wa moyo.

3Wakati misingi imeharibiwa, mwenye haki anaweza kufanya nini?”

4Bwana yuko ndani ya Hekalu lake takatifu; Bwana yuko kwenye kiti chake cha enzi mbinguni. Huwaangalia wana wa watu, macho yake yanawajaribu.

5Bwana huwajaribu wenye haki, lakini waovu na wanaopenda jeuri, nafsi yake huwachukia.

6Atawanyeshea waovu makaa ya moto mkali na kiberiti kinachowaka, upepo wenye joto kali ndio fungu lao.

7Kwa kuwa Bwana ni mwenye haki, yeye hupenda haki. Wanyofu watauona uso wake.

Zaburi

Open the interactive reader to switch translations, adjust type, and mark verses — or browse verses by topic.

Neno: Bibilia Takatifu — Kiswahili Contemporary Version. Copyright © 1984, 1989, 2009, 2015 Biblica, Inc. Used under the Biblica Open (Toleo Wazi) License. · Biblica Open License