Zaburi 123

Neno: Kiswahili Contemporary Version

Ninayainua macho yangu kwako, kwako wewe ambaye kiti chako cha enzi kiko mbinguni.

Kama vile macho ya watumwa yatazamavyo mkono wa bwana wao, kama vile macho ya mtumishi wa kike yatazamavyo mkono wa bibi yake, ndivyo macho yetu yamtazamavyo Bwana Mungu wetu, mpaka atakapotuhurumia.

Uturehemu, Ee Bwana, uturehemu, kwa maana tumevumilia dharau nyingi.

Tumevumilia dhihaka nyingi kutoka kwa wenye kiburi, dharau nyingi kutoka kwa wenye majivuno.

Zaburi

Fungua msomaji shirikishi ili kubadilisha tafsiri, kurekebisha herufi, na kutia alama mistari — au vinjari mistari kwa mada.

Neno: Bibilia Takatifu — Kiswahili Contemporary Version. Copyright © 1984, 1989, 2009, 2015 Biblica, Inc. Used under the Biblica Open (Toleo Wazi) License. · Biblica Open License