Zaburi 54

Neno: Kiswahili Contemporary Version

1Ee Mungu uniokoe kwa jina lako, unifanyie hukumu kwa uwezo wako.

2Ee Mungu, sikia maombi yangu, usikilize maneno ya kinywa changu.

3Wageni wananishambulia, watu wakatili wanayatafuta maisha yangu, watu wasiomjali Mungu.

4Hakika Mungu ni msaada wangu, Bwana ndiye anayenitegemeza.

5Mabaya na yawarudie wale wanaonisingizia, kwa uaminifu wako uwaangamize.

6Nitakutolea dhabihu za hiari; Ee Bwana, nitalisifu jina lako kwa kuwa ni vyema.

7Kwa maana ameniokoa katika shida zangu zote, na macho yangu yamewatazama adui zangu kwa ushindi.

Zaburi

Open the interactive reader to switch translations, adjust type, and mark verses — or browse verses by topic.

Neno: Bibilia Takatifu — Kiswahili Contemporary Version. Copyright © 1984, 1989, 2009, 2015 Biblica, Inc. Used under the Biblica Open (Toleo Wazi) License. · Biblica Open License