1 Mambo ya Nyakati 1
Open Word Bible
Adamu, Sethi, Enoshi, Kenani, Mahalaleli, Yaredi, Henoko, Methusela, Lameki, Nuhu, Shemu, Hamu na Yafethi.
Wana wa Yafethi: Gomeri, Magogu, Madai, Yavani, Tubali, Mesheki na Tirasi.
Wana wa Gomeri: Ashkenazi, Difathi na Togarma. Wana wa Yavani: Elisha, Tarshishi, Wakitimu na Warodanimu.
Wana wa Hamu: Kushi, Misri, Puti na Kanaani. Wana wa Kushi: Seba, Havila, Sabta, Raama na Sabteka. Wana wa Raama: Sheba na Dedani.
Kushi alikuwa baba wa Nimrodi, aliyekuwa shujaa mkuu wa kwanza duniani.
Misri alikuwa babu wa Waludi, Waanami, Walehabi, Wanaftuhi, Wapathrusi, Wakasluhi (ambao ndio asili ya Wafilisti) na Wakaftori.
Kanaani alikuwa baba wa Sidoni, mzaliwa wake wa kwanza, na wa Hethi, na wa Wayebusi, Waamori, Wagirgashi, Wahivi, Waarki, Wasini, Waarvadi, Wasemari na Wahamathi.
Wana wa Shemu: Elamu, Ashuru, Arfaksadi, Ludi, Aramu, Usi, Huli, Getheri na Mesheki.
Arfaksadi alikuwa baba wa Shela, na Shela alikuwa baba wa Eberi. Wana wawili walizaliwa kwa Eberi. Mmoja aliitwa Pelegi, kwa sababu wakati wake dunia iligawanyika. Ndugu yake aliitwa Yoktani. Yoktani alikuwa baba wa Almodadi, Shelefu, Hasarmawethi, Yera, Hadoramu, Uzali, Dikla, Ebali, Abimaeli, Sheba, Ofiri, Havila na Yobabu. Hao wote walikuwa wana wa Yoktani.
Shemu, Arfaksadi, Shela, Eberi, Pelegi, Reu, Serugi, Nahori, Tera, Abramu, yaani Abrahamu.
Wana wa Abrahamu: Isaka na Ishmaeli.
Hii ndiyo orodha ya ukoo wao: Nebayothi, mzaliwa wa kwanza wa Ishmaeli, kisha Kedari, Adbeeli, Mibsamu, Mishma, Duma, Masa, Hadadi, Tema, Yeturi, Nafishi na Kedema. Hao ndio waliokuwa wana wa Ishmaeli.
Wana wa Ketura, suria wa Abrahamu: alimzaa Zimrani, Yokshani, Medani, Midiani, Ishbaki na Shua. Wana wa Yokshani: Sheba na Dedani.
Wana wa Midiani: Efa, Eferi, Hanoki, Abida na Eldaa. Hao wote walikuwa wazao wa Ketura.
Abrahamu alikuwa baba wa Isaka. Wana wa Isaka: Esau na Israeli.
Wana wa Esau: Elifazi, Reueli, Yeushi, Yalamu na Kora.
Wana wa Elifazi: Temani, Omari, Sefi, Gatamu, Kenazi, Timna na Amaleki.
Wana wa Reueli: Nahathi, Zera, Shama na Miza.
Wana wa Seiri: Lotani, Shobali, Sibeoni, Ana, Dishoni, Ezeri na Dishani. Wana wa Lotani: Hori na Homamu. Dada yake Lotani alikuwa Timna.
Wana wa Shobali: Aliani, Manahathi, Ebali, Shefi na Onamu. Wana wa Sibeoni: Aya na Ana. Wana wa Ana: Dishoni. Wana wa Dishoni: Hamrani, Eshbani, Ithrani na Kerani.
Wana wa Ezeri: Bilhani, Zaavani na Yaakani. Wana wa Dishani: Usi na Arani.
Hawa ndio wafalme waliotawala nchi ya Edomu kabla mfalme yeyote hajawatawala Waisraeli: Bela mwana wa Beori, ambaye mji wake uliitwa Dinhaba. Bela alipokufa, Yobabu mwana wa Zera, wa Bosra, akawa mfalme mahali pake. Yobabu alipokufa, Hushamu wa nchi ya Watemani akawa mfalme mahali pake. Hushamu alipokufa, Hadadi mwana wa Bedadi akawa mfalme mahali pake; yeye ndiye aliyewashinda Wamidiani katika nchi ya Moabu. Mji wake uliitwa Avithi. Hadadi alipokufa, Samla wa Masreka akawa mfalme mahali pake. Samla alipokufa, Shauli wa Rehobothi iliyo kando ya Mto akawa mfalme mahali pake. Shauli alipokufa, Baal-hanani mwana wa Akbori akawa mfalme mahali pake. Baal-hanani alipokufa, Hadadi akawa mfalme mahali pake. Mji wake uliitwa Pai, na mke wake alikuwa Mehetabeli, binti Matredi, mjukuu wa Mezahabu. Kisha Hadadi akafa. Wakuu wa Edomu walikuwa Timna, Alva, Yethethi, Oholibama, Ela, Pinoni, Kenazi, Temani, Mibsari, Magdieli na Iramu. Hao ndio waliokuwa wakuu wa Edomu.
1 Mambo ya Nyakati
Fungua msomaji shirikishi ili kubadilisha tafsiri, kurekebisha herufi, na kutia alama mistari — au vinjari mistari kwa mada.
Manukuu ya Maandiko yametoka katika Open Word Bible, ambayo iko katika uwanja wa umma.