Mistari ya Biblia Kuhusu Dhuluma

Mistari 13 ya Biblia kuhusu Dhuluma ya kusoma, kutafakari, na kuikariri.

01 Isaya 1:17

jifunzeni kutenda mema! Tafuteni haki, watieni moyo walioonewa. Teteeni shauri la yatima, wateteeni wajane.

02 Zaburi 9:9

Bwana ni kimbilio la watu wanaoonewa, ni ngome imara wakati wa shida.

03 Zaburi 103:6

Bwana hutenda haki, naye huwapa hukumu ya haki wote wanaoonewa.

04 Mhubiri 4:1

Nikatazama tena nikaona uonevu wote uliokuwa unafanyika chini ya jua: Nikaona machozi ya walioonewa, wala hawana wa kuwafariji; uwezo ulikuwa upande wa wale wanaowaonea, wala hawana wa kuwafariji.

05 Zekaria 7:10

Msimwonee mjane wala yatima, mgeni wala maskini. Msiwaziane mabaya mioyoni mwenu ninyi kwa ninyi.’

06 Mithali 22:22-23

Usiwadhulumu maskini kwa sababu ni maskini, wala kumdhulumu mhitaji mahakamani, kwa sababu Bwana atalichukua shauri lao naye atawateka wao waliowateka.

07 Zaburi 12:5

“Kwa sababu ya uonevu wa wanyonge na kulia kwa uchungu kwa wahitaji, nitainuka sasa,” asema Bwana. “Nitawalinda kutokana na wale wenye nia mbaya juu yao.”

08 Zaburi 72:4

Atawatetea walioonewa miongoni mwa watu na atawaokoa watoto wa wahitaji, ataponda mdhalimu.

09 Isaya 10:1-2

Ole wao wawekao sheria zisizo za haki, kwa wale watoao amri za kuonea, kuwanyima maskini haki zao na kuzuilia haki za watu wangu walioonewa, kuwafanya wajane mawindo yao na kuwanyangʼanya yatima.

10 Mithali 14:31

Yeye amwoneaye maskini huonyesha dharau kwa Muumba wao, bali yeyote anayemhurumia mhitaji humheshimu Mungu.

11 Zaburi 146:7

Naye huwapatia haki walioonewa na kuwapa wenye njaa chakula. Bwana huwaweka wafungwa huru,

12 Yeremia 22:3

Hili ndilo Bwana asemalo: Tenda haki na adili. Mwokoe mkononi mwa mdhalimu yeye aliyetekwa nyara. Usimtendee mabaya wala ukatili mgeni, yatima au mjane, wala usimwage damu isiyo na hatia mahali hapa.

13 Amosi 5:11

Mnamgandamiza maskini na kumlazimisha awape nafaka. Kwa hiyo, ingawa mmejenga majumba ya mawe ya fahari, hamtaishi ndani yake; ingawa mmepanda mashamba mazuri ya mizabibu, hamtakunywa divai yake.

Mada zinazohusiana