Mistari ya Biblia Kuhusu Mjane

Mistari 14 ya Biblia kuhusu Mjane ya kusoma, kutafakari, na kuikariri.

01 Zaburi 68:5

Baba wa yatima, mtetezi wa wajane, ni Mungu katika makao yake matakatifu.

02 Yakobo 1:27

Dini iliyo safi, isiyo na uchafu, inayokubalika mbele za Mungu Baba yetu, ndiyo hii: Kuwasaidia yatima na wajane katika dhiki zao na kujilinda usitiwe madoa na dunia.

03 Kumbukumbu 10:18

Huwapigania yatima na wajane, humpenda mgeni, akimpa chakula na mavazi.

04 Isaya 1:17

jifunzeni kutenda mema! Tafuteni haki, watieni moyo walioonewa. Teteeni shauri la yatima, wateteeni wajane.

05 Kutoka 22:22

“Usimdhulumu mjane wala yatima.

06 Zaburi 146:9

Bwana huwalinda wageni na kuwategemeza yatima na wajane, lakini hupinga njia za waovu.

07 Kumbukumbu 24:19

Unapovuna shamba lako na ukasahau mganda, usirudi kuuchukua. Acha kwa ajili ya mgeni, yatima na mjane, ili Bwana Mungu wako aweze kukubariki wewe katika kazi zote za mikono yako.

08 1 Timotheo 5:3

Waheshimu wanawake wajane ambao ni wajane kweli kweli.

09 Yeremia 49:11

Waache yatima wako; nitayalinda maisha yao. Wajane wako pia wanaweza kunitumaini mimi.”

10 Zekaria 7:10

Msimwonee mjane wala yatima, mgeni wala maskini. Msiwaziane mabaya mioyoni mwenu ninyi kwa ninyi.’

11 Mithali 15:25

Bwana hubomoa nyumba ya mtu mwenye kiburi, bali huilinda mipaka ya mjane isiguswe.

12 Luka 7:13

Bwana Yesu alipomwona yule mjane, moyo wake ulimhurumia, akamwambia, “Usilie.”

13 Kumbukumbu 14:29

ili Walawi (ambao hawana mashamba wala urithi wao wenyewe) na wageni, yatima na wajane wanaoishi kwenye miji yenu wapate kuja kula na kushiba, ili Bwana Mungu wenu apate kuwabariki ninyi katika kazi zote za mikono yenu.

14 Marko 12:42-43

Lakini mjane mmoja maskini akaja na kuweka sarafu mbili ndogo za shaba zenye thamani ya senti mbili. Yesu akawaita wanafunzi wake, akawaambia, “Amin, nawaambia, huyu mjane maskini ameweka katika sanduku la hazina zaidi ya watu wengine wote.

Mada zinazohusiana