Mistari ya Biblia Kuhusu Ukarimu kwa Maskini
Mistari 6 ya Biblia kuhusu Ukarimu kwa Maskini ya kusoma, kutafakari, na kuikariri.
Watu wakarimu watabarikiwa, kwa sababu huwagawia maskini chakula chao.
Anayemhurumia maskini anamkopesha BWANA, naye atamlipa kwa yale aliyoyatenda.
Yeyote anayewapa maskini hatakosa kitu, lakini yeyote anayegeuza macho yake mbali nao atapata laana nyingi.
Badala yake, unapofanya karamu, waalike maskini, walemavu wa viungo, viwete na vipofu. Nawe utakuwa mwenye heri, kwa maana wao hawana njia ya kukulipa. Malipo yako yatakuja wakati wa ufufuo wa wenye haki.”
Kama Maandiko yasemavyo: “Ametawanya vipawa vyake kila mahali, amewapa wahitaji; haki yake inadumu milele.”
Kwa kila njia nimewaonyesha mfano: kwa kufanya kazi kwa bidii hivi, ni lazima tuwasaidie walio dhaifu, na tuyakumbuke maneno ya Bwana Yesu, jinsi yeye mwenyewe alivyosema, ‘Kutoa kuna heri kubwa zaidi kuliko kupokea.’”