Mistari ya Biblia Kuhusu Kuwatetea Wanyonge

Mistari 6 ya Biblia kuhusu Kuwatetea Wanyonge ya kusoma, kutafakari, na kuikariri.

Ongeza mistari yote 6 Fungua akaunti ya bure ili kuikariri.
01 Zaburi 82:3 Mstari mkuu

Wahukumuni kwa haki wanyonge na yatima; watangazeni wanaoteseka na fukara kuwa hawana hatia.

02 Mithali 31:8-9

Fungua kinywa chako kwa ajili ya wale wasio na sauti, kwa ajili ya shauri la wote walioachwa waangamie. Sema waziwazi na uhukumu kwa haki; chukua shauri la maskini na la mhitaji.”

03 Zaburi 72:4

Na awatetee maskini kati ya watu, na kuziokoa jamaa za wahitaji; na amvunjevunje mdhalimu.

04 Zaburi 82:4

Wapelekeni wanyonge na maskini mahali salama; wanyakueni kutoka katika mshiko wa waovu.

05 Mithali 24:11-12

Waokoe wanaoburutwa kwenda kuuawa; wazuie wale wanaojikokota kuelekea machinjoni. Ukisema, “Lakini sisi hatukujua lolote juu ya jambo hili,” je, yeye apimaye mioyo haoni ukweli? Yeye aulindaye uhai wako anajua vizuri, naye atamlipa kila mtu kwa kadiri ya alichotenda.

06 Zaburi 41:1

Wana heri kweli wale wanaowajali wanyonge! Taabu inapokuja, BWANA atawaokoa.

Mada zinazohusiana