Mistari ya Biblia Kuhusu Haki

Mistari 11 ya Biblia kuhusu Haki ya kusoma, kutafakari, na kuikariri.

01 Mika 6:8

Amekuonyesha yaliyo mema, ee mwanadamu. Bwana anataka nini kwako? Ila kutenda kwa haki na kupenda rehema, na kwenda kwa unyenyekevu na Mungu wako.

02 Isaya 1:17

jifunzeni kutenda mema! Tafuteni haki, watieni moyo walioonewa. Teteeni shauri la yatima, wateteeni wajane.

03 Amosi 5:24

Lakini acheni haki itiririke kama mto, na uadilifu uwe kama kijito kisichokauka!

04 Mithali 21:3

Kufanya yaliyo sawa na haki inakubalika zaidi kwa Bwana kuliko dhabihu.

05 Kumbukumbu 16:20

Mfuate haki na haki peke yake, ili mweze kuishi na kuimiliki nchi ambayo Bwana Mungu wenu anawapa.

06 Zekaria 7:9

“Hivi ndivyo asemavyo Bwana Mwenye Nguvu Zote: ‘Fanyeni hukumu za haki, onyesheni rehema na huruma ninyi kwa ninyi.

07 Zaburi 33:5

Bwana hupenda uadilifu na haki; dunia imejaa upendo wake usiokoma.

08 Isaya 30:18

Hata hivyo Bwana anatamani kutupatia neema, anainuka ili kuwaonyesha huruma. Kwa kuwa Bwana ni Mungu wa haki. Wamebarikiwa wote wanaomngojea yeye!

09 Mithali 31:9

Sema na uamue kwa haki, tetea haki za maskini na wahitaji.”

10 Yeremia 22:3

Hili ndilo Bwana asemalo: Tenda haki na adili. Mwokoe mkononi mwa mdhalimu yeye aliyetekwa nyara. Usimtendee mabaya wala ukatili mgeni, yatima au mjane, wala usimwage damu isiyo na hatia mahali hapa.

11 Zaburi 106:3

Heri wale wanaodumisha haki, ambao daima wanafanya yaliyo mema.

Mada zinazohusiana