Mistari ya Biblia Kuhusu Maskini
Mistari 14 ya Biblia kuhusu Maskini ya kusoma, kutafakari, na kuikariri.
Yeye amhurumiaye maskini humkopesha Bwana, naye atamtuza kwa aliyotenda.
Yeye amwoneaye maskini huonyesha dharau kwa Muumba wao, bali yeyote anayemhurumia mhitaji humheshimu Mungu.
Heri mtu yule anayemjali mnyonge, Bwana atamwokoa wakati wa shida.
Walichotuomba ni kwamba tuendelee kuwakumbuka maskini, jambo ambalo ndilo nililokuwa na shauku ya kulifanya.
Yeye ampaye maskini hatapungukiwa na kitu chochote, bali yeye awafumbiaye maskini macho hupata laana nyingi.
Najua kwamba Bwana huwapatia maskini haki, na kuitegemeza njia ya mhitaji.
Bali ufanyapo karamu, waalike maskini, vilema na vipofu,
Mtu mkarimu yeye mwenyewe atabarikiwa kwa kuwa hushiriki chakula chake na maskini.
Mwenye haki hujali haki kwa ajili ya maskini, bali mwovu hajishughulishi na hilo.
Ikiwa kuna mtu maskini miongoni mwa ndugu zenu, katika mji wowote wa hiyo nchi ambayo Bwana Mungu wenu anawapa, msiwe na moyo mgumu wala usimfumbie mkono ndugu yako aliye maskini. Afadhali fungua mikono yako na umkopeshe kwa hiari chochote anachohitaji.
Huwainua maskini kutoka mavumbini, na kuwanyanyua wahitaji kutoka kwenye jalala,
“Roho wa Bwana yu juu yangu, kwa sababu amenitia mafuta kuwahubiria maskini habari njema. Amenituma kuwatangazia wafungwa kufunguliwa kwao, na vipofu kupata kuona tena, kuwaweka huru wanaoonewa,
Ndugu zangu, sikilizeni: Je, Mungu hakuwachagua wale walio maskini machoni pa ulimwengu kuwa matajiri katika imani na kuurithi Ufalme aliowaahidi wale wampendao?
Sema na uamue kwa haki, tetea haki za maskini na wahitaji.”