Mistari ya Biblia Kuhusu Yatima
Mistari 12 ya Biblia kuhusu Yatima ya kusoma, kutafakari, na kuikariri.
Dini iliyo safi, isiyo na uchafu, inayokubalika mbele za Mungu Baba yetu, ndiyo hii: Kuwasaidia yatima na wajane katika dhiki zao na kujilinda usitiwe madoa na dunia.
Baba wa yatima, mtetezi wa wajane, ni Mungu katika makao yake matakatifu.
Huwapigania yatima na wajane, humpenda mgeni, akimpa chakula na mavazi.
Ashuru hawezi kutuokoa, hatutapanda farasi wa vita. Kamwe hatutasema tena ‘Miungu yetu’ kwa kile ambacho mikono yetu wenyewe imetengeneza, kwa kuwa kwako wewe yatima hupata huruma.”
Lakini wewe, Ee Mungu, unaona shida na huzuni, umekubali kuyapokea mkononi mwako. Mhanga anajisalimisha kwako, wewe ni msaada wa yatima.
Bwana huwalinda wageni na kuwategemeza yatima na wajane, lakini hupinga njia za waovu.
“Usimdhulumu mjane wala yatima.
Waache yatima wako; nitayalinda maisha yao. Wajane wako pia wanaweza kunitumaini mimi.”
jifunzeni kutenda mema! Tafuteni haki, watieni moyo walioonewa. Teteeni shauri la yatima, wateteeni wajane.
Usipotoshe hukumu ya mgeni au yatima, au kuchukua vazi la mjane kama rehani.
Hata kama baba yangu na mama wakiniacha, Bwana atanipokea.
Msimwonee mjane wala yatima, mgeni wala maskini. Msiwaziane mabaya mioyoni mwenu ninyi kwa ninyi.’