Mistari ya Biblia Kuhusu Mtwike Mungu Mahangaiko Yako

Mistari 12 ya Biblia kuhusu Mtwike Mungu Mahangaiko Yako ya kusoma, kutafakari, na kuikariri.

Ongeza mistari yote 12 Fungua akaunti ya bure ili kuikariri.
01 1 Petro 5:7 Mstari mkuu

Fanyeni hivyo kwa kumtupia yeye kila wasiwasi mlio nao, kwa sababu ninyi ni wa thamani kwake.

02 Wafilipi 4:6-7

Msiwe na wasiwasi kuhusu jambo lolote. Badala yake, katika kila jambo, mpelekeeni Mungu haja zenu kwa sala na maombi, pamoja na shukrani. Na amani ya Mungu, iliyo juu ya ufahamu wetu wote, itailinda kama mlinzi mioyo yenu na mawazo yenu katika Kristo Yesu.

03 Zaburi 55:22

Mkabidhi BWANA kila kinachokulemea, na yeye atakutegemeza; kamwe yeye hatamwacha mwenye haki ajikwae na kuanguka.

04 Mathayo 11:28-30

Njooni kwangu, nyote mliochoshwa na kazi ngumu na kuelemewa na mizigo mizito, nami nitawapa pumziko. Vaeni nira yangu shingoni mwenu, mjifunze kutoka kwangu, kwa kuwa ni mpole na moyo wangu ni mnyenyekevu. Ndipo mtakapopata pumziko kwa nafsi zenu. Kwa maana nira yangu haiumizi kuivaa, na mzigo ninaowapa ni mwepesi.”

05 Zaburi 56:3

Siku hofu inaponishika, nitakutegemea wewe.

06 Zaburi 37:5

Mwachie BWANA mwelekeo wa maisha yako; umtegemee, naye ataingilia kati.

07 Mathayo 6:25

Ndiyo sababu nawaambia: msiwe na wasiwasi kuhusu uhai wenu, kwamba mtakula nini, wala kuhusu miili yenu, kwamba mtavaa nini. Je, uhai si wa thamani kuliko chakula, na mwili kuliko mavazi?

08 Zaburi 62:8

Enyi watu, mtegemeeni yeye kila wakati; mwagieni mioyo yenu mbele yake. Mungu ni kimbilio letu. Sela

09 Mithali 3:5-6

Mwamini BWANA kwa moyo wako mzima, wala usijiegemeze kwenye busara yako mwenyewe. Mkumbuke yeye katika kila unalofanya, naye atakutengenezea njia iliyonyooka mbele yako.

10 Zaburi 94:19

Wasiwasi unaponisonga, faraja yako hunijaza furaha.

11 Zaburi 42:5

Mbona umeinama hivyo, nafsi yangu? Mbona huku kuhangaika ndani yangu? Mngojee Mungu kwa tumaini; nitamshukuru tena, kwa wokovu unaotoka mbele zake.

12 Yohana 14:27

Amani ninawaachia; ni amani yangu mwenyewe ninayowapa. Sitoi kama ulimwengu unavyotoa. Mioyo yenu isifadhaike, wala isikubali kushindwa na hofu.

Mada zinazohusiana