Mistari ya Biblia Kuhusu Mateso
Mistari 12 ya Biblia kuhusu Mateso ya kusoma, kutafakari, na kuikariri.
Kwa maana dhiki yetu nyepesi iliyo ya kitambo inatutayarisha kwa ajili ya utukufu wa milele unaozidi kuwa mwingi kupita kiasi,
Mwenye haki ana mateso mengi, lakini Bwana humwokoa nayo yote,
Nasi tunajua ya kuwa katika mambo yote Mungu hutenda kazi pamoja na wote wampendao, katika kuwapatia mema, yaani, wale walioitwa kwa kusudi lake.
Twataabika kila upande lakini hatuangamizwi; twaona wasiwasi lakini hatukati tamaa; twateswa lakini hatuachwi; twatupwa chini lakini hatupondwi.
Ilikuwa vyema mimi kupata shida ili nipate kujifunza maagizo yako.
Faraja yangu katika mateso yangu ni hii: Ahadi yako inahifadhi maisha yangu.
Bwana yu karibu na waliovunjika moyo, na huwaokoa waliopondeka roho.
Bwana ni kimbilio la watu wanaoonewa, ni ngome imara wakati wa shida.
Kabla sijapata shida nilipotea njia, lakini sasa ninalitii neno lako.
Ingawa huleta huzuni, ataonyesha huruma, kwa kuwa upendo wake usiokoma ni mkuu. Kwa maana hapendi kuwaletea mateso au huzuni watoto wa wanadamu.
“Heri mtu yule ambaye Mungu humrudi; kwa hiyo usidharau adhabu yake Mwenyezi.
Bwana ni Mwema, kimbilio wakati wa taabu. Huwatunza wale wanaomtegemea,