Mistari ya Biblia Kuhusu Bonde

Mistari 6 ya Biblia kuhusu Bonde ya kusoma, kutafakari, na kuikariri.

01 Zaburi 23:4

Hata kama nikipita katikati ya bonde la uvuli wa mauti, sitaogopa mabaya, kwa maana wewe upo pamoja nami; fimbo yako na mkongojo wako vyanifariji.

02 Zaburi 23:1-3

Bwana ndiye mchungaji wangu, sitapungukiwa na kitu. Hunilaza katika malisho ya majani mabichi, kando ya maji matulivu huniongoza, hunihuisha nafsi yangu. Huniongoza katika njia za haki kwa ajili ya jina lake.

03 Isaya 43:2

Unapopita kwenye maji makuu, nitakuwa pamoja nawe, unapopita katika mito ya maji, hayatakugharikisha. Utakapopita katika moto, hutaungua, miali ya moto haitakuunguza.

04 Zaburi 46:1-2

Mungu kwetu sisi ni kimbilio na nguvu, msaada utakaoonekana tele wakati wa mateso. Kwa hiyo hatutaogopa, hata kama dunia ikiondolewa nayo milima ikiangukia moyoni mwa bahari.

05 Zaburi 84:6

Wanapopita katika Bonde la Baka, hulifanya mahali pa chemchemi, pia mvua za vuli hulijaza kwa madimbwi.

06 Zaburi 23:5

Waandaa meza mbele yangu machoni pa adui zangu. Umenipaka mafuta kichwani pangu, kikombe changu kinafurika.

Mada zinazohusiana