Mistari ya Biblia Kuhusu Ugonjwa

Mistari 7 ya Biblia kuhusu Ugonjwa ya kusoma, kutafakari, na kuikariri.

01 Yakobo 5:14-15

Je, kuna yeyote miongoni mwenu aliye mgonjwa? Basi inampasa awaite wazee wa kanisa wamwombee na kumpaka mafuta kwa Jina la Bwana. Kule kuomba kwa imani kutamwokoa huyo mgonjwa, naye Bwana atamwinua na kama ametenda dhambi, atasamehewa.

02 Zaburi 41:3

Bwana atamtegemeza awapo mgonjwa kitandani, atamwinua kutoka kitandani mwake.

03 Mathayo 8:16-17

Jioni ile, wakamletea watu wengi waliopagawa na pepo wachafu, naye akawatoa wale pepo wachafu kwa neno lake, na kuwaponya wagonjwa wote. Haya yalifanyika ili litimie lile lililonenwa kwa kinywa cha nabii Isaya kwamba: “Mwenyewe alitwaa udhaifu wetu na alichukua magonjwa yetu.”

04 Isaya 53:4

Hakika alichukua udhaifu wetu na akajitwika huzuni zetu, hata hivyo tulidhania kuwa amepigwa na Mungu, akapigwa sana naye, na kuteswa.

05 Zaburi 103:2-3

Ee nafsi yangu, umhimidi Bwana, wala usisahau wema wake wote, akusamehe dhambi zako zote, akuponya magonjwa yako yote,

06 Zaburi 38:9

Ee Bwana, yote ninayoyaonea shauku yako wazi mbele zako, kutamani kwangu sana hakufichiki mbele zako.

07 Marko 2:17

Yesu aliposikia haya akawaambia, “Watu wenye afya hawahitaji tabibu, bali walio wagonjwa. Sikuja kuwaita wenye haki, bali wenye dhambi.”

Mada zinazohusiana