Mistari ya Biblia Kuhusu Kutegemezwa
Mistari 15 ya Biblia kuhusu Kutegemezwa ya kusoma, kutafakari, na kuikariri.
Mtwike Bwana fadhaa zako, naye atakutegemeza, hatamwacha kamwe mwenye haki wake aanguke.
Hivyo usiogope, kwa maana niko pamoja nawe; usifadhaike, kwa maana mimi ni Mungu wako. Nitakutia nguvu na kukusaidia; nitakutegemeza kwa mkono wa kuume wa haki yangu.
Hakika Mungu ni msaada wangu, Bwana ndiye anayenitegemeza.
Hata mpaka wakati wa uzee wenu na mvi, Mimi ndiye, Mimi ndiye nitakayewasaidia ninyi. Nimewahuluku, nami nitawabeba, nitawasaidia ninyi na kuwaokoa.
Hunipa ngao yako ya ushindi, nao mkono wako wa kuume hunitegemeza, unajishusha chini ili kuniinua.
Ninajilaza na kupata usingizi; naamka tena, kwa maana Bwana hunitegemeza.
bali wale wamtumainio Bwana atafanya upya nguvu zao. Watapaa juu kwa mbawa kama tai; watapiga mbio wala hawatachoka, watatembea kwa miguu wala hawatazimia.
Bwana huwategemeza wote waangukao, na huwainua wote waliolemewa na mizigo yao.
Mungu wa milele ni kimbilio lako, na chini kuna mikono ya milele. Atamfukuza adui yako mbele yako, akisema, ‘Mwangamize yeye!’
ajapojikwaa, hataanguka, kwa maana Bwana humtegemeza kwa mkono wake.
Nihifadhi sawasawa na ahadi yako, nami nitaishi; usiache matumaini yangu yakavunjwa.
Kwa sababu ya upendo mkuu wa Bwana, hatuangamii, kwa kuwa huruma zake hazikomi kamwe. Ni mpya kila asubuhi, uaminifu wako ni mkuu.
Niliposema, “Mguu wangu unateleza,” Ee Bwana, upendo wako ulinishikilia.
Kwa miaka arobaini uliwatunza jangwani. Hawakukosa chochote, na nguo zao hazikuchakaa wala miguu yao haikuvimba.
Hatauacha mguu wako uteleze, yeye akulindaye hatasinzia,