Mistari ya Biblia Kuhusu Kimbilio

Mistari 13 ya Biblia kuhusu Kimbilio ya kusoma, kutafakari, na kuikariri.

01 Zaburi 46:1

Mungu kwetu sisi ni kimbilio na nguvu, msaada utakaoonekana tele wakati wa mateso.

02 Zaburi 62:8

Enyi watu, mtumainini yeye wakati wote, miminieni mioyo yenu kwake, kwa kuwa Mungu ni kimbilio letu.

03 Mithali 18:10

Jina la Bwana ni ngome imara, wenye haki huikimbilia na kuwa salama.

04 Zaburi 9:9

Bwana ni kimbilio la watu wanaoonewa, ni ngome imara wakati wa shida.

05 Nahumu 1:7

Bwana ni Mwema, kimbilio wakati wa taabu. Huwatunza wale wanaomtegemea,

06 Zaburi 91:2

Nitasema kumhusu Bwana, “Yeye ndiye kimbilio langu na ngome yangu, Mungu wangu, ambaye ninamtumaini.”

07 Zaburi 18:2

Bwana ni mwamba wangu, ngome yangu na mwokozi wangu, Mungu wangu ni mwamba, ambaye kwake ninakimbilia. Yeye ni ngao yangu na pembe ya wokovu wangu, ngome yangu.

08 Zaburi 32:7

Wewe ndiwe mahali pangu pa kujificha, utaniepusha na taabu na kunizunguka kwa nyimbo za wokovu.

09 Zaburi 61:3-4

Kwa kuwa umekuwa kimbilio langu, ngome imara dhidi ya adui. Natamani kukaa hemani mwako milele, na kukimbilia chini ya uvuli wa mbawa zako.

10 Zaburi 142:5

Ee Bwana, nakulilia wewe, nasema, “Wewe ni kimbilio langu, fungu langu katika nchi ya walio hai.”

11 Kumbukumbu 33:27

Mungu wa milele ni kimbilio lako, na chini kuna mikono ya milele. Atamfukuza adui yako mbele yako, akisema, ‘Mwangamize yeye!’

12 Zaburi 31:1-2

Ee Bwana, nimekukimbilia wewe, usiache nikaaibika kamwe, kwa haki yako uniokoe. Nitegee sikio lako, uje uniokoe haraka; uwe kwangu mwamba wa kimbilio, ngome imara ya kuniokoa.

13 2 Samweli 22:3

Mungu wangu ni mwamba wangu, ambaye kwake ninakimbilia, ngao yangu na pembe ya wokovu wangu. Yeye ni ngome yangu, kimbilio langu na mwokozi wangu, huniokoa kutoka kwa watu wenye jeuri.

Mada zinazohusiana