Mistari ya Biblia Kuhusu Mungu Ngao Yetu
Mistari 8 ya Biblia kuhusu Mungu Ngao Yetu ya kusoma, kutafakari, na kuikariri.
BWANA ni nguvu yangu, ngao inayonilinda; moyo wangu ulimtumaini, nami nikapata msaada. Sasa moyo wangu umejaa furaha, nami nitamshukuru kwa wimbo.
Muda fulani baadaye, neno la BWANA lilimjia Abramu katika maono: “Abramu, usiogope. Ngao yako ni mimi, nawe utapata thawabu kubwa sana.”
Lakini wewe, Ee BWANA, ni ngao kila upande wangu. Wewe ni utukufu wangu, na unakiinua kichwa changu tena.
Huyu ndiye Mungu: njia yake haina dosari; neno la BWANA limejaribiwa na ni la kweli; yeye ni ngao kwa wote wanaomfanya kuwa kimbilio lao.
Kila neno asemalo Mungu limethibitika kuwa kweli; yeye ni ngao kwa wote wanaokimbilia kwake.
Kwa maana BWANA Mungu ni jua na ngao; BWANA hutoa neema na heshima; wale waendao bila lawama hawanyimi kitu chochote chema.
Kwa nafsi zetu zote tunamngojea BWANA; yeye ndiye anayetusaidia na kutukinga kama ngao.
Kwako ninapata mahali pa kujificha na ngao yangu; tumaini langu limewekwa kwenye neno lako.