Mistari ya Biblia Kuhusu Ulinzi

Mistari 7 ya Biblia kuhusu Ulinzi ya kusoma, kutafakari, na kuikariri.

01 Zaburi 91:1-2

Yeye akaaye mahali pa salama pake Yeye Aliye Juu Sana, atadumu katika uvuli wake Mwenyezi. Nitasema kumhusu Bwana, “Yeye ndiye kimbilio langu na ngome yangu, Mungu wangu, ambaye ninamtumaini.”

02 Zaburi 121:7-8

Bwana atakukinga na madhara yote, atayalinda maisha yako, Bwana atakulinda unapoingia na unapotoka, tangu sasa na hata milele.

03 Isaya 41:10

Hivyo usiogope, kwa maana niko pamoja nawe; usifadhaike, kwa maana mimi ni Mungu wako. Nitakutia nguvu na kukusaidia; nitakutegemeza kwa mkono wa kuume wa haki yangu.

Lakini Bwana ni mwaminifu, naye atawaimarisha ninyi na kuwalinda kutokana na yule mwovu.

05 Zaburi 32:7

Wewe ndiwe mahali pangu pa kujificha, utaniepusha na taabu na kunizunguka kwa nyimbo za wokovu.

06 Zaburi 121:1-3

Nayainua macho yangu nitazame vilima, msaada wangu utatoka wapi? Msaada wangu hutoka kwa Bwana, Muumba wa mbingu na dunia. Hatauacha mguu wako uteleze, yeye akulindaye hatasinzia,

07 Mithali 18:10

Jina la Bwana ni ngome imara, wenye haki huikimbilia na kuwa salama.

Mada zinazohusiana