Mistari ya Biblia Kuhusu Silaha za Mungu

Mistari 9 ya Biblia kuhusu Silaha za Mungu ya kusoma, kutafakari, na kuikariri.

01 Waefeso 6:11

Vaeni silaha zote za Mungu ili kwamba mweze kuzipinga hila za ibilisi.

02 Waefeso 6:13

Kwa hiyo vaeni silaha zote za Mungu ili mweze kushindana siku ya uovu itakapokuja nanyi mkiisha kufanya yote, simameni imara.

03 Waefeso 6:14-15

Kwa hiyo simameni imara mkiwa mmejifunga kweli kiunoni na kuvaa dirii ya haki kifuani, nayo miguu yenu ifungiwe utayari tuupatao kwa Injili ya amani.

04 Waefeso 6:16

Zaidi ya haya yote, twaeni ngao ya imani, ambayo kwa hiyo mtaweza kuizima mishale yote yenye moto ya yule mwovu.

05 2 Wakorintho 10:4

Silaha za vita vyetu si za mwili, bali zina uwezo katika Mungu hata kuangusha ngome,

06 Waefeso 6:12

Kwa maana kushindana kwetu si juu ya nyama na damu, bali dhidi ya falme, mamlaka, dhidi ya wakuu wa giza na majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho.

07 Waefeso 6:18

Mkiomba kwa Roho siku zote katika sala zote na maombi, mkikesha kila wakati mkiwaombea watakatifu wote.

08 Warumi 13:12

Usiku umeendelea sana, mapambazuko yamekaribia. Kwa hiyo tuyaweke kando matendo ya giza na tuvae silaha za nuru.

Lakini kwa kuwa sisi ni wana wa mchana, basi tuwe na kiasi, tukijivika imani na upendo kama dirii kifuani na tumaini letu la wokovu kama chapeo.

Mada zinazohusiana