Mistari ya Biblia Kuhusu Ukombozi wa Mateso
Mistari 9 ya Biblia kuhusu Ukombozi wa Mateso ya kusoma, kutafakari, na kuikariri.
Wenye haki wanapolia, BWANA husikiliza na kuwaweka huru kutoka katika kila taabu inayowapata.
BWANA ni jabali langu, ngome yangu, yule anayeniweka huru; Mungu wangu ni mwamba wangu, nami ninajificha kwake. Yeye ni ngao yangu, wokovu wangu wenye nguvu, mnara wangu juu milimani.
Mungu alituokoa kutoka katika kifo kikubwa namna hiyo, naye atatuokoa. Tumeweka tumaini letu kwake kwamba atatuokoa tena,
Nilimngojea BWANA, nikaendelea kumngojea, naye akaniinamia na kukisikiliza kilio changu cha kuomba msaada. Alinivuta juu kutoka katika shimo lenye kelele za maji, kutoka katika matope yanayonata; akaipandikiza miguu yangu juu ya mwamba na kuziimarisha hatua zangu.
Nilikwenda kumtafuta BWANA; akanipa jibu na kuniokoa kutoka katika kila kitu nilichokihofia.
Katika dhiki yao walimlilia BWANA, naye akawanasua katika taabu zao.
Bwana ataniokoa kutoka katika kila shambulio ovu, na kunifikisha salama katika ufalme wake wa mbinguni. Utukufu uwe kwake milele na milele. Amina.
na uniite wakati shida zinapokuja; nitakuweka huru, nawe utanipa utukufu.”
Yeye ametuokoa kutoka katika nguvu za giza, akatuleta katika ufalme wa Mwana anayempenda.