Mistari ya Biblia Kuhusu Maombi
Maombi ni pumzi ya maisha ya Kikristo — kuongea na Mungu asikiaye na kujibuye. Msijisumbue kwa neno lo lote; bali katika kila neno kwa kusali na kuomba, pamoja na kushukuru, haja zenu na zijulikane na Mungu. Aya hizi zinakualika kuomba kwa ujasiri na kwa kupumzika.
Msiwe na wasiwasi kuhusu jambo lolote. Badala yake, katika kila jambo, mpelekeeni Mungu haja zenu kwa sala na maombi, pamoja na shukrani.
Basi, kwanza kabisa, nasihi kwamba dua, maombi, maombezi na shukrani zitolewe kwa ajili ya watu wote:
Yesu aliwaambia mfano kuhusu jinsi wanavyopaswa kuomba wakati wote bila kukata tamaa.
Mkikaa ndani yangu na maneno yangu yakakaa ndani yenu, ombeni chochote mnachotaka, nanyi mtafanyiwa.
Wenye haki wanapolia, BWANA husikiliza na kuwaweka huru kutoka katika kila taabu inayowapata.
Hata lini, Ee BWANA? Je, utaendelea kunisahau kabisa? Hata lini utaugeuzia mbali uso wako?
Basi tukaribie kiti cha enzi cha neema tukiwa na ujasiri, ili tupokee rehema na kupata neema inayotuletea msaada wakati ule ule tunapouhitaji.
Endeleeni kuomba, nanyi mtapokea. Endeleeni kutafuta, nanyi mtapata. Endeleeni kubisha hodi, nanyi mtafunguliwa mlango.
Maombi yaliyofanywa kwa imani yatamwokoa mgonjwa, na Bwana atamwinua. Na kama ametenda dhambi, atasamehewa.
Lakini ninyi, wapendwa, endeleeni kujijenga juu ya imani yenu iliyo takatifu kabisa, na kuomba katika Roho Mtakatifu.
Kwa hiyo jengeni desturi ya kuungamiana dhambi na kuombeana, ili mponywe. Mtu mwenye haki anapoomba, ombi lake linafanya kazi, nalo linaweza kutimiza mambo mengi.
Lakini unapoomba, ingia katika chumba cha ndani, ufunge mlango, umwombe Baba yako aliye pale kwa siri. Baba yako huona yaliyofichika, naye atakulipa.
Tena, kweli nawaambia, ikiwa wawili kati yenu hapa duniani watapatana juu ya jambo lolote watakaloliomba, Baba yangu aliye mbinguni atawafanyia.