Mistari ya Biblia Kuhusu Maombezi

Mistari 7 ya Biblia kuhusu Maombezi ya kusoma, kutafakari, na kuikariri.

01 1 Timotheo 2:1

Awali ya yote, nasihi kwamba dua, sala, maombezi na shukrani zifanyike kwa ajili ya watu wote:

02 Yakobo 5:16

Kwa hiyo ungamianeni dhambi zenu ninyi kwa ninyi na kuombeana ili mpate kuponywa. Maombi ya mwenye haki yana nguvu tena yanafaa sana.

03 Waefeso 6:18

Mkiomba kwa Roho siku zote katika sala zote na maombi, mkikesha kila wakati mkiwaombea watakatifu wote.

04 Warumi 8:26

Vivyo hivyo, Roho hutusaidia katika udhaifu wetu, kwa sababu hatujui kuomba ipasavyo. Lakini Roho mwenyewe hutuombea kwa uchungu usioweza kutamkwa.

05 Wakolosai 4:2

Dumuni sana katika maombi, mkikesha katika hayo pamoja na kushukuru.

06 1 Timotheo 2:1-2

Awali ya yote, nasihi kwamba dua, sala, maombezi na shukrani zifanyike kwa ajili ya watu wote: kwa ajili ya wafalme na wale wote wenye mamlaka, ili tupate kuishi kwa amani na utulivu, katika uchaji wote wa Mungu na utakatifu.

07 Ayubu 42:10

Baada ya Ayubu kuwaombea rafiki zake, Bwana akamwondoa kwenye uteka, akamfanikisha tena naye akampa mara mbili ya vile alivyokuwa navyo hapo mwanzoni.

Mada zinazohusiana