Mistari ya Biblia Kuhusu Ombeni bila Kukoma
Mistari 12 ya Biblia kuhusu Ombeni bila Kukoma ya kusoma, kutafakari, na kuikariri.
Msiache kuomba.
Endeleeni kuomba kwa bidii, na mkeshe mnapoomba, huku mkishukuru.
Ombeni katika Roho kila wakati unaofaa, kwa kila aina ya sala na dua. Kwa ajili hiyo, kaeni macho, msikate tamaa kamwe, na mwaombee watu wote wa Mungu walio watakatifu.
Yesu aliwaambia mfano kuhusu jinsi wanavyopaswa kuomba wakati wote bila kukata tamaa.
Tumaini lenu liwape furaha daima; vumilieni katika dhiki; msiache kuomba.
Wote hao walijitoa kwa bidii kwa maombi, wakiwa na nia moja. Pamoja nao walikuwepo wale wanawake, Mariamu mama wa Yesu, na ndugu zake.
Walijitoa kikamilifu kwa mafundisho ya mitume na kwa maisha ya kushirikiana, kwa kumega mkate pamoja na kwa maombi.
Jioni, asubuhi na adhuhuri ninamweleza taabu zangu na kuugua kwa sauti, na yeye ananisikia.
Mgeukieni BWANA na nguvu zake; njooni mbele zake tena na tena.
Msiwe na wasiwasi kuhusu jambo lolote. Badala yake, katika kila jambo, mpelekeeni Mungu haja zenu kwa sala na maombi, pamoja na shukrani.
Sisi tutashikamana na maombi na huduma ya neno.”
Mungu, ninayemtumikia kwa roho yangu yote katika kuhubiri Injili ya Mwana wake, anaweza kushuhudia jinsi ninavyowakumbuka daima