Mistari ya Biblia Kuhusu Kumlilia Mungu

Mistari 8 ya Biblia kuhusu Kumlilia Mungu ya kusoma, kutafakari, na kuikariri.

01 Zaburi 34:17

Wenye haki hulia, naye Bwana huwasikia, huwaokoa katika taabu zao zote.

02 Zaburi 18:6

Katika shida yangu nalimwita Bwana, nilimlilia Mungu wangu anisaidie. Kutoka hekaluni mwake alisikia sauti yangu, kilio changu kikafika mbele zake, masikioni mwake.

03 Zaburi 120:1

Katika dhiki yangu namwita Bwana, naye hunijibu.

04 Yona 2:2

Akasema: “Katika shida yangu nalimwita Bwana, naye akanijibu. Kutoka kina cha kaburi niliomba msaada, nawe ukasikiliza kilio changu.

05 Zaburi 145:18

Bwana yu karibu na wote wamwitao, karibu na wote wamwitao kwa uaminifu.

06 Zaburi 40:1

Nilimngoja Bwana kwa saburi, naye akaniinamia, akasikia kilio changu.

07 Zaburi 86:7

Katika siku ya shida yangu nitakuita, kwa maana wewe utanijibu.

08 Zaburi 77:1

Nilimlilia Mungu ili anisaidie, nilimlilia Mungu ili anisikie.

Mada zinazohusiana