Mistari ya Biblia Kuhusu Kudumu katika Maombi

Mistari 10 ya Biblia kuhusu Kudumu katika Maombi ya kusoma, kutafakari, na kuikariri.

01 Luka 18:1

Kisha Yesu akawapa wanafunzi wake mfano ili kuwaonyesha kuwa yawapasa kuomba pasipo kukata tamaa.

02 Luka 11:9-10

“Kwa hiyo nawaambia: Ombeni nanyi mtapewa; tafuteni nanyi mtapata; bisheni nanyi mtafunguliwa mlango. Kwa kuwa kila aombaye hupewa; naye kila atafutaye hupata; na kila abishaye hufunguliwa mlango.

03 Wakolosai 4:2

Dumuni sana katika maombi, mkikesha katika hayo pamoja na kushukuru.

04 Warumi 12:12

Kuweni na furaha katika tumaini, katika dhiki kuweni na saburi, dumuni katika maombi.

05 Luka 18:7

Je, Mungu hatawatendea haki wateule wake wanaomlilia usiku na mchana? Je, atakawia kuwasaidia?

06 Luka 11:8

Nawaambia, ingawa huyo mtu hataamka na kumpa hiyo mikate kwa sababu ni rafiki yake, lakini kwa sababu ya kuendelea kwake kuomba, ataamka na kumpa kiasi anachohitaji.

07 Waefeso 6:18

Mkiomba kwa Roho siku zote katika sala zote na maombi, mkikesha kila wakati mkiwaombea watakatifu wote.

ombeni bila kukoma;

09 Luka 18:5

lakini kwa kuwa huyu mjane ananisumbuasumbua, nitahakikisha amepata haki yake ili asiendelee kunichosha kwa kunijia mara kwa mara!’ ”

10 Mwanzo 32:26

Ndipo yule mtu akasema, “Niache niende, kwa kuwa ni mapambazuko.” Lakini Yakobo akajibu, “Sitakuacha uende usiponibariki.”

Mada zinazohusiana