Mistari ya Biblia Kuhusu Kupatana katika Maombi

Mistari 6 ya Biblia kuhusu Kupatana katika Maombi ya kusoma, kutafakari, na kuikariri.

Ongeza mistari yote 6 Fungua akaunti ya bure ili kuikariri.
01 Mathayo 18:19 Mstari mkuu

Tena, kweli nawaambia, ikiwa wawili kati yenu hapa duniani watapatana juu ya jambo lolote watakaloliomba, Baba yangu aliye mbinguni atawafanyia.

02 Mathayo 18:20

Kwa kuwa popote wanapokutana wawili au watatu kwa jina langu, nipo hapo pamoja nao.”

03 Matendo 1:14

Wote hao walijitoa kwa bidii kwa maombi, wakiwa na nia moja. Pamoja nao walikuwepo wale wanawake, Mariamu mama wa Yesu, na ndugu zake.

04 Matendo 2:42

Walijitoa kikamilifu kwa mafundisho ya mitume na kwa maisha ya kushirikiana, kwa kumega mkate pamoja na kwa maombi.

05 Matendo 4:24

Waliposikia habari hiyo, wote kwa pamoja wakapaza sauti zao kwa Mungu, wakaomba, “Bwana Mkuu, Muumba wa mbingu na nchi, na wa bahari, na wa vyote vilivyomo!

06 Matendo 12:5

Kwa hiyo Petro alikuwa akilindwa gerezani, lakini kanisa lilikuwa likimwomba Mungu kwa ajili yake bila kukoma.

Mada zinazohusiana