Mistari ya Biblia Kuhusu Ombi la Imani

Mistari 9 ya Biblia kuhusu Ombi la Imani ya kusoma, kutafakari, na kuikariri.

Ongeza mistari yote 9 Fungua akaunti ya bure ili kuikariri.
01 Yakobo 5:15 Mstari mkuu

Maombi yaliyofanywa kwa imani yatamwokoa mgonjwa, na Bwana atamwinua. Na kama ametenda dhambi, atasamehewa.

02 Marko 11:24

Kwa hiyo nawaambia: chochote mnachoomba mnaposali, aminini kwamba mmekipokea, nanyi mtakipata.

03 Yakobo 1:6

Lakini aombe kwa imani, bila kusitasita. Mtu anayesitasita ni kama wimbi la bahari kuu, linalosukumwa na upepo na kutupwa huku na huku.

04 Mathayo 21:22

Na chochote mtakachoomba katika maombi mtakipokea, ilimradi mnaamini.”

05 Waebrania 11:6

Na hakuna anayeweza kumpendeza Mungu bila imani, kwa sababu kila anayemkaribia Mungu hana budi kuamini kwamba yeye yuko, na pia kwamba huwalipa wale wanaomtafuta kwa bidii.

06 Mathayo 17:20

Aliwaambia, “Ni kwa sababu imani yenu ni ndogo mno. Kweli nawaambia, kama mna imani hata iliyo ndogo kama mbegu ya haradali, mnaweza kuuambia mlima huu, ‘Toka hapa uende pale,’ nao utakwenda. Hakuna jambo ambalo hamtaweza kulifanya.”

07 Marko 9:23

Yesu akamwambia, “’Kama unaweza!’ Kila kitu kinawezekana kwa mtu anayeamini.”

08 1 Yohana 5:14-15

Tunapomkaribia tunakuwa na ujasiri huu: kila tunapoomba jambo linalopatana na mapenzi yake, yeye hutusikiliza. Na ikiwa tunajua kwamba anatusikia katika chochote tunachoomba, tunajua kwamba maombi tuliyomwomba ni yetu.

09 Yakobo 1:5

Ikiwa mmoja wenu anakosa hekima, amwombe Mungu, anayewapa watu wote kwa mkono wazi bila kuwasuta, naye atapewa.

Mada zinazohusiana