Mistari ya Biblia Kuhusu Ombi Lenye Nguvu

Mistari 9 ya Biblia kuhusu Ombi Lenye Nguvu ya kusoma, kutafakari, na kuikariri.

Ongeza mistari yote 9 Fungua akaunti ya bure ili kuikariri.
01 Yakobo 5:16 Mstari mkuu

Kwa hiyo jengeni desturi ya kuungamiana dhambi na kuombeana, ili mponywe. Mtu mwenye haki anapoomba, ombi lake linafanya kazi, nalo linaweza kutimiza mambo mengi.

02 Mathayo 21:22

Na chochote mtakachoomba katika maombi mtakipokea, ilimradi mnaamini.”

03 1 Yohana 5:14-15

Tunapomkaribia tunakuwa na ujasiri huu: kila tunapoomba jambo linalopatana na mapenzi yake, yeye hutusikiliza. Na ikiwa tunajua kwamba anatusikia katika chochote tunachoomba, tunajua kwamba maombi tuliyomwomba ni yetu.

04 Yohana 15:7

Mkikaa ndani yangu na maneno yangu yakakaa ndani yenu, ombeni chochote mnachotaka, nanyi mtafanyiwa.

05 Marko 11:24

Kwa hiyo nawaambia: chochote mnachoomba mnaposali, aminini kwamba mmekipokea, nanyi mtakipata.

06 Mathayo 7:7-8

Endeleeni kuomba, nanyi mtapokea. Endeleeni kutafuta, nanyi mtapata. Endeleeni kubisha hodi, nanyi mtafunguliwa mlango. Kwa maana kila anayeomba hupokea, yeyote anayetafuta hupata, na anayebisha hodi hufunguliwa mlango.

07 Wafilipi 4:6-7

Msiwe na wasiwasi kuhusu jambo lolote. Badala yake, katika kila jambo, mpelekeeni Mungu haja zenu kwa sala na maombi, pamoja na shukrani. Na amani ya Mungu, iliyo juu ya ufahamu wetu wote, itailinda kama mlinzi mioyo yenu na mawazo yenu katika Kristo Yesu.

08 Waebrania 4:16

Basi tukaribie kiti cha enzi cha neema tukiwa na ujasiri, ili tupokee rehema na kupata neema inayotuletea msaada wakati ule ule tunapouhitaji.

09 Luka 11:9-10

Basi nawaambia: ombeni, na Mungu atawapa; tafuteni, na mtapata; bisheni hodi, na Mungu atawafungulia mlango. Kwa maana wote wanaoomba hupokea, wote wanaotafuta hupata, na wote wanaobisha hodi watafunguliwa mlango.

Mada zinazohusiana