Mistari ya Biblia Kuhusu Nyumbani

Mistari 12 ya Biblia kuhusu Nyumbani ya kusoma, kutafakari, na kuikariri.

Ongeza mistari yote 12 Fungua akaunti ya bure ili kuikariri.
01 Yoshua 24:15 Mstari mkuu

Ikiwa kumtumikia BWANA kunaonekana vibaya kwenu, basi fanyeni uchaguzi wenu leo. Mtamtumikia nani? Miungu ambayo babu zenu waliitumikia upande wa pili wa Mto, au miungu ya Waamori ambao sasa mnaishi katika nchi yao? Mimi na watu wa nyumbani mwangu tutamtumikia BWANA.”

02 Zaburi 127:1

Wimbo wa kupanda. Wa Sulemani. Ikiwa BWANA si yeye anayejenga nyumba, kazi ya wajenzi wake inakuwa bure. Ikiwa BWANA haulindi mji, kukesha kwa mlinzi usiku kucha ni bure.

03 Mithali 24:3-4

Nyumba hujengwa kwa hekima na kuthibitishwa kwa ufahamu; kwa maarifa vyumba vyake hujazwa kila aina ya hazina ya thamani na nzuri.

04 Mithali 14:1

Mwanamke mwenye hekima hujenga nyumba yake, bali mpumbavu huibomoa kwa mikono yake mwenyewe.

05 Matendo 16:31

Wakamjibu, “Mwamini Bwana Yesu, nawe utaokolewa, wewe pamoja na watu wa nyumbani mwako.”

Yaandike kwenye miimo ya milango ya nyumba yako na kwenye malango ya mji wako.

07 Mithali 12:7

Waovu hupinduliwa wakatoweka, bali nyumba ya wenye haki itasimama imara.

08 Mithali 15:6

Nyumba ya mwenye haki ina hazina kubwa, bali mapato ya mwovu huleta taabu.

09 Zaburi 128:3

Ndani kabisa ya nyumba yako mke wako atakuwa kama mzabibu uliojaa zabibu, na kuizunguka meza yako watoto wako watakuwa kama mimea michanga ya mizeituni.

10 Mithali 31:27

Huchunga kwa makini yote yanayoendelea nyumbani mwake; kamwe hali chakula asichokifanyia kazi.

11 1 Timotheo 5:8

Mtu yeyote asiyewatunza jamaa zake, na hasa watu wa nyumbani mwake, ameikana imani, naye ni mbaya kuliko mtu asiyeamini.

12 Zaburi 101:2

Nitajitahidi kuishika njia isiyo na lawama. Utakuja kwangu lini? Ndani ya nyumba yangu mwenyewe nitaishi kwa moyo usiogawanyika.

Mada zinazohusiana