Mistari ya Biblia Kuhusu Watoto
Mistari 9 ya Biblia kuhusu Watoto ya kusoma, kutafakari, na kuikariri.
Wana ni urithi utokao kwa Bwana, watoto ni zawadi kutoka kwake.
Yesu akasema, “Waacheni watoto wadogo waje kwangu, wala msiwazuie, kwa maana Ufalme wa Mbinguni ni wa wale walio kama hawa.”
Kama mishale mikononi mwa shujaa ndivyo walivyo wana awazaao mtu katika ujana wake. Heri mtu ambaye podo lake limejazwa nao. Hawataaibishwa wanaposhindana na adui zao langoni.
Akawachukua watoto mikononi mwake, akawakumbatia, akaweka mikono yake juu yao, akawabariki.
Wana wa wana ni taji la wazee, nao wazazi ni fahari ya watoto wao.
Yesu alipoona yaliyokuwa yakitukia, akachukizwa. Akawaambia wanafunzi wake, “Waacheni watoto wadogo waje kwangu, wala msiwazuie, kwa maana Ufalme wa Mungu ni wa wale walio kama hawa.
Wafundishe watoto wako kwa bidii. Nena kuhusu amri hizi uketipo nyumbani na wakati utembeapo njiani, ulalapo na uamkapo.
Mfundishe mtoto njia impasayo kuiendea, naye hataiacha hata akiwa mzee.
“Yeyote amkaribishaye mtoto mdogo kama huyu kwa Jina langu, anikaribisha mimi.