Mistari ya Biblia Kuhusu Malezi

Mistari 12 ya Biblia kuhusu Malezi ya kusoma, kutafakari, na kuikariri.

01 Waefeso 6:4

Ninyi akina baba, msiwachokoze watoto wenu, bali waleeni kwa nidhamu na mafundisho ya Bwana.

02 Mithali 22:6

Mfundishe mtoto njia impasayo kuiendea, naye hataiacha hata akiwa mzee.

03 Kumbukumbu 6:6-7

Amri hizi ninazokupa leo zitakuwa katika moyo wako. Wafundishe watoto wako kwa bidii. Nena kuhusu amri hizi uketipo nyumbani na wakati utembeapo njiani, ulalapo na uamkapo.

04 Zaburi 127:3

Wana ni urithi utokao kwa Bwana, watoto ni zawadi kutoka kwake.

05 Mithali 29:17

Mrudi mwanao, naye atakupa amani, atakufurahisha nafsi yako.

06 Mithali 13:24

Yeye aizuiaye fimbo yake hampendi mwanawe, bali yeye ampendaye huwa mwangalifu kumwadibisha.

07 Mithali 22:15

Upumbavu umefungwa ndani ya moyo wa mtoto, bali fimbo ya adhabu itaufukuzia mbali naye.

08 Zaburi 78:4-6

Hatutayaficha kwa watoto wao; tutakiambia kizazi kijacho matendo yastahiliyo sifa ya Bwana, uweza wake, na maajabu aliyoyafanya. Aliagiza amri kwa Yakobo na akaweka sheria katika Israeli, ambazo aliwaamuru baba zetu wawafundishe watoto wao, ili kizazi kijacho kizijue, pamoja na watoto ambao watazaliwa, nao pia wapate kuwaeleza watoto wao.

09 Mithali 19:18

Mrudi mwanao, kwa maana katika hiyo kuna tumaini, usiwe mshirika katika mauti yake.

10 2 Timotheo 3:15

na jinsi ambavyo tangu utoto umeyajua Maandiko matakatifu, ambayo yanaweza kukuhekimisha upate wokovu kwa njia ya imani katika Kristo Yesu.

11 Mithali 20:11

Hata mtoto hujulikana kwa matendo yake, kama tabia yake ni safi na adili.

12 Wakolosai 3:21

Ninyi akina baba, msiwachokoze watoto wenu, wasije wakakata tamaa.

Mada zinazohusiana