Mistari ya Biblia Kuhusu Kulea Watoto Wamchao Mungu

Mistari 12 ya Biblia kuhusu Kulea Watoto Wamchao Mungu ya kusoma, kutafakari, na kuikariri.

01 Mithali 22:6

Mfundishe mtoto njia impasayo kuiendea, naye hataiacha hata akiwa mzee.

02 Kumbukumbu 6:6-7

Amri hizi ninazokupa leo zitakuwa katika moyo wako. Wafundishe watoto wako kwa bidii. Nena kuhusu amri hizi uketipo nyumbani na wakati utembeapo njiani, ulalapo na uamkapo.

03 Waefeso 6:4

Ninyi akina baba, msiwachokoze watoto wenu, bali waleeni kwa nidhamu na mafundisho ya Bwana.

04 Zaburi 78:4

Hatutayaficha kwa watoto wao; tutakiambia kizazi kijacho matendo yastahiliyo sifa ya Bwana, uweza wake, na maajabu aliyoyafanya.

05 Mithali 29:17

Mrudi mwanao, naye atakupa amani, atakufurahisha nafsi yako.

06 Mithali 22:15

Upumbavu umefungwa ndani ya moyo wa mtoto, bali fimbo ya adhabu itaufukuzia mbali naye.

07 Mithali 13:24

Yeye aizuiaye fimbo yake hampendi mwanawe, bali yeye ampendaye huwa mwangalifu kumwadibisha.

08 2 Timotheo 1:5

Nimekuwa nikiikumbuka imani yako ya kweli, waliokuwa nayo bibi yako Loisi na mama yako Eunike na ambayo mimi ninasadiki sasa wewe pia unayo.

09 Mithali 1:8-9

Mwanangu, sikiliza mwongozo wa baba yako, wala usiyaache mafundisho ya mama yako. Hayo yatakuwa taji la maua la neema kichwani pako, na mkufu wa kuipamba shingo yako.

10 Isaya 54:13

Watoto wako wote watafundishwa na Bwana, nayo amani ya watoto wako itakuwa kuu.

11 Kumbukumbu 4:9

Mwe waangalifu, na makini ili msije mkasahau mambo ambayo mliyaona kwa macho yenu, wala kuyaacha yaondoke moyoni mwenu siku zote za uhai wenu. Mwafundishe hayo watoto wenu na watoto wao baada yao.

12 3 Yohana 1:4

Sina furaha kubwa kuliko hii, kusikia kwamba watoto wangu wanaenenda katika kweli.

Mada zinazohusiana

Kutoka kwa miongozo