Mistari ya Biblia Kuhusu Kuwaheshimu Wazazi

Mistari 7 ya Biblia kuhusu Kuwaheshimu Wazazi ya kusoma, kutafakari, na kuikariri.

01 Kutoka 20:12

Waheshimu baba yako na mama yako, ili upate kuishi siku nyingi katika nchi anayokupa Bwana Mungu wako.

02 Waefeso 6:1-3

Enyi watoto, watiini wazazi wenu katika Bwana, kwa kuwa hili ni jema. “Waheshimu baba yako na mama yako,” hii ndio amri ya kwanza yenye ahadi, “upate baraka na uishi siku nyingi duniani.”

03 Mithali 23:22

Msikilize baba yako, aliyekuzaa, wala usimdharau mama yako atakapokuwa mzee.

04 Wakolosai 3:20

Enyi watoto, watiini wazazi wenu katika mambo yote, kwa maana hivi ndivyo inavyompendeza Bwana.

05 Mithali 1:8

Mwanangu, sikiliza mwongozo wa baba yako, wala usiyaache mafundisho ya mama yako.

06 Walawi 19:3

“ ‘Kila mmoja wenu ni lazima amheshimu mama yake na baba yake, na pia ni lazima kuzishika Sabato zangu. Mimi ndimi Bwana Mungu wenu.

07 Mithali 6:20

Mwanangu, zishike amri za baba yako, wala usiyaache mafundisho ya mama yako.

Mada zinazohusiana