Mistari ya Biblia Kuhusu Utukufu wa Jina Lake
Mistari 8 ya Biblia kuhusu Utukufu wa Jina Lake ya kusoma, kutafakari, na kuikariri.
Mpeni Bwana utukufu unaostahili jina lake; mwabuduni Bwana katika uzuri wa utakatifu wake.
Ee Bwana, Bwana wetu, tazama jinsi lilivyo tukufu jina lako duniani mwote! Umeuweka utukufu wako juu ya mbingu.
Kwa hiyo, Mungu alimtukuza juu sana, na kumpa Jina lililo kuu kuliko kila jina, ili kwa Jina la Yesu, kila goti lipigwe, la vitu vya mbinguni, na vya duniani, na vya chini ya nchi,
Kuanzia mawio ya jua hadi machweo yake, jina la Bwana linapaswa kusifiwa.
Jina langu litakuwa kuu miongoni mwa mataifa, kuanzia mawio ya jua hata machweo yake. Kila mahali uvumba na sadaka safi zitaletwa kwa Jina langu, kwa sababu Jina langu litakuwa kuu miongoni mwa mataifa,” asema Bwana Mwenye Nguvu Zote.
Mpeni Bwana utukufu unaostahili jina lake; leteni sadaka na mje katika nyua zake.
Katika siku hiyo mtasema: “Mshukuruni Bwana, mliitie jina lake; julisheni miongoni mwa mataifa yale aliyoyafanya, tangazeni kuwa jina lake limetukuka.
Jina lake tukufu lisifiwe milele, ulimwengu wote ujae utukufu wake. Amen na Amen.