Mistari ya Biblia Kuhusu Uzuri wa Mungu

Mistari 11 ya Biblia kuhusu Uzuri wa Mungu ya kusoma, kutafakari, na kuikariri.

01 1 Nyakati 29:11

Ukuu na uweza, ni vyako, Ee Bwana, na utukufu na enzi na uzuri, kwa kuwa kila kilichoko mbinguni na duniani ni chako wewe. Ee Bwana, ufalme ni wako; umetukuzwa kuwa mkuu juu ya yote.

02 Zaburi 104:1

Ee nafsi yangu, umhimidi Bwana. Ee Bwana Mungu wangu, wewe ni mkuu sana, umejivika utukufu na enzi.

03 Zaburi 96:6

Fahari na enzi viko mbele yake; nguvu na utukufu vimo patakatifu pake.

04 Zaburi 145:5

Watasema juu ya utukufu wa fahari ya ukuu wako, nami nitatafakari juu ya kazi zako za ajabu.

05 Zaburi 8:1

Ee Bwana, Bwana wetu, tazama jinsi lilivyo tukufu jina lako duniani mwote! Umeuweka utukufu wako juu ya mbingu.

06 Zaburi 21:5

Kutokana na ushindi uliompa, utukufu wake ni mkubwa, umeweka juu yake fahari na utukufu.

07 Ayubu 37:22

Kutoka kaskazini yeye huja na fahari kuu; Mungu huja katika utukufu wa kutisha.

08 Zaburi 111:3

Kazi zake zimejaa fahari na utukufu, haki yake hudumu daima.

09 Habakuki 3:3-4

Mungu alitoka Temani, yeye Aliye Mtakatifu kutoka Mlima Parani. Utukufu wake ulifunika mbingu, na sifa zake zikaifunika dunia. Mngʼao wake ulikuwa kama jua lichomozalo; mionzi ilimulika kutoka mkononi mwake, ambako nguvu zake zilifichwa.

10 Zaburi 90:16

Matendo yako na yaonekane kwa watumishi wako, utukufu wako kwa watoto wao.

11 Isaya 60:1

“Ondoka, angaza, kwa kuwa nuru yako imekuja na utukufu wa Bwana umezuka juu yako.

Mada zinazohusiana