Mistari ya Biblia Kuhusu Fahari Yake
Mistari 10 ya Biblia kuhusu Fahari Yake ya kusoma, kutafakari, na kuikariri.
Ee BWANA, Bwana wetu, jina lako lina utukufu ulioje duniani kote! Fahari yako inafika juu kuliko mbingu.
BWANA ni Mfalme! Amevaa enzi kama joho; BWANA amejivika, akajifunga nguvu kama mshipi. Ulimwengu umesimama imara; hakuna kitakachoutikisa.
Nafsi yangu, mbariki BWANA. Ee BWANA Mungu wangu, jinsi ulivyo mkuu! Fahari na enzi ndizo mavazi unayovaa,
Ee BWANA, ukuu, uweza, utukufu, ushindi na enzi ni vyako; naam, kila kitu kilicho mbinguni na duniani ni chako. Ufalme ni wako, Ee BWANA, nawe umetukuzwa kuwa kichwa juu ya yote.
kwa Mungu pekee, Mwokozi wetu, kupitia Yesu Kristo Bwana wetu, kuwe na utukufu, adhama, nguvu na mamlaka, tangu kabla ya mwanzo wa wakati, sasa, na milele yote. Amina.
Nitaitafakari enzi yako, utukufu wake na fahari yake, na habari za maajabu yako.
Fahari na enzi vimesimama mbele yake; nguvu na uzuri vimejaa mahali pake patakatifu.
Kwa sababu ulimwokoa, heshima yake iko juu sana; unaweka juu yake fahari ya kifalme na enzi.
Tulipowaambia habari za nguvu za Bwana wetu Yesu Kristo na kuja kwake, hatukuwa tukisimulia hadithi za ujanja zilizobuniwa na watu. Tuliuona ukuu wake kwa macho yetu wenyewe.
Sauti ya BWANA ina nguvu nyingi; sauti ya BWANA ina fahari ya kifalme.