Mistari ya Biblia Kuhusu Bwana Anastahili
Mistari 9 ya Biblia kuhusu Bwana Anastahili ya kusoma, kutafakari, na kuikariri.
“Bwana wetu na Mungu wetu, wewe unastahili kupokea utukufu, heshima na uweza, kwa sababu wewe uliviumba vitu vyote: kwa kuwa ulipenda, vilikuwepo na viliumbwa.”
Walisema kwa sauti kubwa, “Mwanakondoo aliyechinjwa anastahili kupokea uweza, utajiri, hekima, nguvu, heshima, utukufu na sifa!”
BWANA ni mkuu, anastahili sifa za juu kabisa, na hakuna awezaye kuchunguza kina cha ukuu wake.
Ninamwita BWANA, anayestahili kusifiwa, nami ninaokolewa kutoka kwa adui zangu.
Wanaimba wimbo mpya: “Wewe unastahili kulipokea gombo na kuivunja mihuri yake, kwa sababu ulichinjwa, na kwa gharama ya damu yako uliwanunua kwa ajili ya Mungu watu wa kila kabila na lugha na jamii na taifa.
Kisha nilisikia kila kiumbe mbinguni, duniani, chini ya dunia na baharini, na vyote vilivyomo, vikisema: “Kwa yeye aliyeketi juu ya kiti cha enzi na kwa Mwanakondoo kuwe na sifa na heshima na utukufu na uweza milele na milele!”
Ninamwita BWANA, anayestahili kusifiwa, nami ninaokolewa kutoka kwa adui zangu.
Kwa maana BWANA ni mkuu na anastahili sifa kuu kuliko zote; yeye anapaswa kuheshimiwa kwa hofu kuliko kila mungu.
Kwa maana BWANA ni mkuu na anastahili sifa kuu kuliko zote; yeye anapaswa kuheshimiwa kwa hofu kuliko kila mungu.