Mistari ya Biblia Kuhusu Kumcha Bwana
Mistari 6 ya Biblia kuhusu Kumcha Bwana ya kusoma, kutafakari, na kuikariri.
01 Mithali 9:10
“Kumcha Bwana ndicho chanzo cha hekima, na kumjua Aliye Mtakatifu ni ufahamu.
02 Mithali 1:7
Kumcha Bwana ndicho chanzo cha maarifa, lakini wapumbavu hudharau hekima na adabu.
Kumcha Bwana ndicho chanzo cha hekima, wote wanaozifuata amri zake wana busara. Sifa zake zadumu milele.
Kumcha Bwana ni chemchemi ya uzima, ili kumwepusha mtu na mitego ya mauti.
Hii ndiyo jumla ya maneno; yote yamekwisha sikiwa: Mche Mungu, nawe uzishike amri zake, maana kwa jumla ndiyo impasayo mtu.
Kumcha Bwana huongoza kwenye uzima, kisha mtu hupumzika akiwa ameridhika, bila kuguswa na shida.