Mistari ya Biblia Kuhusu Maneno ya Kutia Moyo
Mistari 8 ya Biblia kuhusu Maneno ya Kutia Moyo ya kusoma, kutafakari, na kuikariri.
Neno lililooza lisipite midomoni mwenu. Semeni tu yaliyo mema, yanayojenga na kukidhi hitaji la wakati huo, ili maneno yenu yawaletee neema wale wanaoyasikia.
Wasiwasi huulemea moyo, bali neno la upole huuinua.
Basi endeleeni kutiana moyo na kujengana, kama mnavyofanya tayari.
Badala yake, mtiane moyo siku kwa siku, maadamu bado kuna “Leo,” ili dhambi isimdanganye yeyote kati yenu na kumfanya mgumu.
Maneno ya upole ni sega la asali, matamu kinywani na afya kwa mwili.
Kama matofaa ya dhahabu yaliyowekwa katika fedha, ndivyo lilivyo neno linalosemwa wakati unaofaa kabisa.
Mazungumzo yenu yawe ya upole na ya kupendeza siku zote, yamekolezwa kwa chumvi, ili mjue jinsi ya kumjibu kila mtu.
Kutoa jibu zuri ni furaha, na neno kwa wakati unaofaa, jinsi lilivyo jema!