Mistari ya Biblia Kuhusu Kusema Kweli
Mistari 11 ya Biblia kuhusu Kusema Kweli ya kusoma, kutafakari, na kuikariri.
Badala yake, tukiambiana kweli kwa upendo, katika mambo yote tukue, hata tumfikie yeye aliye kichwa, yaani, Kristo.
Haya ndiyo mtakayoyafanya: Semeni kweli kila mtu kwa mwenzake, na mtoe hukumu ya kweli na haki kwenye mahakama zenu,
Kwa hiyo kila mmoja wenu avue uongo na kuambiana kweli mtu na jirani yake, kwa maana sisi sote tu viungo vya mwili mmoja.
Bwana anachukia sana midomo idanganyayo, bali hufurahia watu ambao ni wa kweli.
Ni yule aendaye pasipo mawaa, atendaye yaliyo haki, asemaye kweli toka moyoni mwake,
Midomo isemayo kweli hudumu milele, bali ulimi wa uongo hudumu kwa muda mfupi tu.
Ndipo mtaijua kweli nayo kweli itawaweka huru.”
Msiambiane uongo, kwa maana mmevua kabisa utu wenu wa kale pamoja na matendo yake,
basi auzuie ulimi wake na mabaya, na midomo yake kutokana na kusema uongo.
Kwa maana, “Yeyote apendaye uzima na kuona siku njema, basi auzuie ulimi wake usinene mabaya, na midomo yake isiseme hila.
Kinywa changu husema lililo kweli, kwa maana midomo yangu huchukia uovu.