Mistari ya Biblia Kuhusu Ulimi

Mistari 7 ya Biblia kuhusu Ulimi ya kusoma, kutafakari, na kuikariri.

Ongeza mistari yote 7 Fungua akaunti ya bure ili kuikariri.
01 Yakobo 3:5 Mstari mkuu

Kwa namna hiyohiyo, ulimi ni sehemu ndogo ya mwili, lakini unajigamba kwa mambo makubwa. Tazama jinsi mwali mdogo unavyoweza kuunguza msitu mkubwa kiasi hicho!

02 Mithali 18:21

Ulimi una uwezo wa uzima na wa kifo, na wanaopenda kusema watakula matunda yake.

03 Yakobo 3:6

Ulimi nao ni moto. Umesimama kati ya viungo vya mwili wetu kama ulimwengu mzima wa udhalimu: unautia doa mwili wote, unawasha moto mwenendo mzima wa maisha, na wenyewe unawashwa moto na Jehanamu.

04 Yakobo 1:26

Mtu akijiona kuwa mcha Mungu lakini hauwekei ulimi wake hatamu, anajidanganya mwenyewe, na dini yake ni tupu.

05 Mithali 21:23

Anayechunga kinywa chake na ulimi wake hujilinda asiingie taabuni.

06 Mithali 15:4

Maneno ya upole ni mti wa uzima, bali ulimi uliopotoka huiponda roho.

07 Waefeso 4:29

Neno lililooza lisipite midomoni mwenu. Semeni tu yaliyo mema, yanayojenga na kukidhi hitaji la wakati huo, ili maneno yenu yawaletee neema wale wanaoyasikia.

Mada zinazohusiana