Mistari ya Biblia Kuhusu Bidii
Mistari 7 ya Biblia kuhusu Bidii ya kusoma, kutafakari, na kuikariri.
Mikono yenye bidii itatawala, bali uvivu huishia katika kazi za utumwa.
02 Mithali 10:4
Mikono mivivu hufanya mtu kuwa maskini lakini mikono yenye bidii huleta utajiri.
Lolote mfanyalo, fanyeni kwa moyo kama watu wanaomtumikia Bwana, na si wanadamu,
04 Mithali 13:4
Mvivu hutamani sana na hapati kitu, bali nafsi ya mwenye bidii hutoshelezwa kikamilifu.
05 Mhubiri 9:10
Lolote mkono wako upatalo kufanya, fanya kwa nguvu zako zote, kwa kuwa huko kuzimu, unakokwenda, hakuna kufanya kazi wala mipango wala maarifa wala hekima.
06 Mithali 21:5
Mipango ya mwenye bidii huelekeza kwenye faida, kama vile kwa hakika pupa huelekeza kwenye umaskini.
Je, unamwona mtu stadi katika kazi yake? Atahudumu mbele ya wafalme; hatahudumu mbele ya watu duni.