Mistari ya Biblia Kuhusu Umaskini

Mistari 12 ya Biblia kuhusu Umaskini ya kusoma, kutafakari, na kuikariri.

01 Mithali 19:17

Yeye amhurumiaye maskini humkopesha Bwana, naye atamtuza kwa aliyotenda.

02 Mithali 14:31

Yeye amwoneaye maskini huonyesha dharau kwa Muumba wao, bali yeyote anayemhurumia mhitaji humheshimu Mungu.

03 Mithali 22:2

Tajiri na maskini wanafanana kwa hili: Bwana ni Muumba wao wote.

04 1 Samweli 2:7

Bwana humfanya mtu maskini naye hutajirisha, hushusha na hukweza.

05 Zaburi 140:12

Najua kwamba Bwana huwapatia maskini haki, na kuitegemeza njia ya mhitaji.

06 Mithali 30:8-9

Uutenge mbali nami udanganyifu na uongo; usinipe umaskini wala utajiri, bali unipe chakula cha kunitosha kila siku. Nisije nikawa na vingi vya kuzidi nikakukana na kusema, ‘ Bwana ni nani?’ Au nisije nikawa maskini nikaiba, nami nikaliaibisha jina la Mungu wangu.

07 Mithali 13:23

Shamba la mtu maskini laweza kuzalisha chakula kingi, bali dhuluma hukifutilia mbali.

08 Mithali 17:5

Yeye anaye mdhihaki maskini huonyesha dharau kwa Muumba wake; yeyote afurahiaye maafa hataepuka kuadhibiwa.

09 Mithali 31:20

Huwanyooshea maskini mikono yake na kuwakunjulia wahitaji vitanga vyake.

10 Luka 6:20

Akawatazama wanafunzi wake, akasema: “Mmebarikiwa ninyi mlio maskini, kwa sababu Ufalme wa Mungu ni wenu.

11 Mithali 21:13

Mtu akiziba masikio asisikie kilio cha maskini, yeye pia atalia, wala hatajibiwa.

12 Mithali 30:14

wale ambao meno yao ni panga na ambao mataya yao yamewekwa visu kuwaangamiza maskini katika nchi, na wahitaji kutoka miongoni mwa wanadamu.

Mada zinazohusiana